Michezo

Aussems athibitisha Tshabalala na Kapombe warejea

on

Baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Mwadui FC kwa kufungwa 1-0 katika uwanja wa Kambarage Shinyanga ukiwa ndio mchezo wake wa kwanza kupoteza msimu huu kati ya 7.

Simba SC Jumapili ya Novemba 3 2019 itakuwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kucheza mchzo wao wa nane wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City, kuelekea mchezo huo kocha wa Simba SC Patrick Aussems amethibitisha kuwa Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Shomary Kapombe wamerejea uwanjani baada ya kupona majeraha.

Sasa ni wazi Aussems anesema Tshabalala na Kapombe wanaweza kutumika kwani wamepona, Simba inaongoza Ligi kwa kuwa na point 18 ikishinda mechi 6 na kupoteza moja.

Soma na hizi

Tupia Comments