fB insta twitter

Tuhuma za ushemeji wa Waziri Jenister Mhagama, Tanzanite One zamtia matatani Millya

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.

May 25 2016 tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine, moja ya habari kubwa ni kutoka Gazeti la Jambo Leo  lenye kichwa cha habari ‘Ushemeji wa Mhagama, Tanzanite One wamtia matatani Mbunge Millya’.

Gazeti hilo limeeleza kuwa tuhuma za ushemeji kati ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenester Mhagama na mmoja wa wabia wa Kampuni ya Sky Associates inayomiliki Mgodi wa Tanzanite One zimelisukuma Bunge kumpa siku nne Mbunge wa Simanjiro ‘CHADEMA’ James Ole Millya athibitishe madai yake kwa ushahidi.

Gazeti hilo limeieleza nukuu ya maneno ya Millya alipokuwa akitoa madai hayo alipokuwa akichangia mjadala bungeni iliyonukuliwa na Naibu Spika, Dk. Tulia ….>>>Sheria za kazi zinajulikana, ni bahati mbaya kwamba Mhagama anatajwa kwamba ni shemeji wa mmoja wa wabia wa hapo. Dada anaitwa Asia Gonga ameolewa na Martin au Yusuph Mhagama’

ULIIKOSA HII YA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE ILIVYOOKOA HIZI MILIONI AMBAZO ZINGETUMIKA KWA MATIBABU NJE YA NCHI ? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUB

Soma na hizi

Tupia Comments