Michezo

Kilimanjaro Stars yadhihirisha kuwa inataka kutetea Kombe lake la CECAFA

on

Mabingwa watetezi wa CECAFA WOMEN SENIOR CHALLENGE timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake Twiga Stars baada ya ushindi wa kishindo wa 9-0 dhidi ta Sudan Kusini leo iliwageukia Burundi.

Twiga Stars ambao ndio Mabingwa watetezi wa michuano hiyo leo wamecheza mchezo wao wa pili wa Kundi A dhidi ya timu ya taifa ya Burundi katika uwanja wa Chamazi na kuibuka na ushindi mnono wa 4-0.

Magoli yakifungwa na Donisia Daniel dakika ya 35 na 65, nahodha wao Asha Rashid na Mwanahamisi Omary dakika ya 86, hadi sasa Twiga Stars inayoongoza Kundi A kwa kuwa na point 6 haijaruhusu kufungwa goli hata moja.

VIDEO: Ikitokea Taifa Stars ikacheza vs England, Bongozozo ataamua hivi dhidi ya taifa lake

Soma na hizi

Tupia Comments