Stori Pekee

Hawa watoto wamepishana miezi miwili kuzaliwa, eti nao wanaitwa mapacha?

on

preg

Watoto hawa wanaweza kuitwa mapacha wa miujiza baada ya kuwashangaza madaktari kutokana na kupishana kwao muda wa kuzaliwa.

Watoto hao walizaliwa katika moja ya hospitali huko Romania, sio kwamba wametofautiana miezi miwili kuzaliwa pia wametofautiana miaka kwani mmoja alizaliwa November 2014, mama huyo alilazimika kukaa chumba cha kujifungulia hadi Januari 2015 ndipo akazaliwa mtoto mwingine.

Madaktari walishangazwa na hali hiyo kwa kuwa si ya kawaida, walitegemea watoto hao wangezaliwa siku moja kama ilivyo kawaida lakini haikuwa hivyo.

Kwa mujibu wa wataalamu walisema watoto hao walizaliwa katika mifuko tofauti ya uzazi ambayo iliruhusu mmoja kuzaliwa kabla ya mwenzake.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments