fB insta twitter

‘Mfungwa adaiwa kuuawa kwa kipigo’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la JamboLeo yenye kichwa cha habari ‘Mfungwa adaiwa kuuawa kwa kipigo’

Gazeti hilo limeripoti kuwa mfungwa namba 79 ya mwaka 2016 John Okol, anadaiwa kuuawa kwa kipigo cha Mkuu wa Gereza la Keko, Kamishna Msaidizi Abdallah Kiange.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka kwa ndugu wa marehemu  zilidai kuwa kifo cha ndugu yao kilichangiwa na kipigo cha Mkuu huyo kwa kilichodaiwa Okol na wenzake wanatumia simu gerezani, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, ndugu hao walidai kuwa tuhuma kwamba wafungwa hao wanatumia simu gerezani zinapaswa kuelekezwa kwa askari Magereza wanaowalinda na kuwa watumishi hao ndio huuzia simu wafungwa.

Kupitia gazeti hilo ndugu walisema zipo taaarifa kuwa wanaohusika na uingizaji wa simu gerezani na kuwauzia wafungwa ni askari wa kikosi cha ukaguzi. Taarifa kutoka ndani ya gereza hilo zilieleza kwamba baada ya tukio la kupigwa na kuwa na hali mbaya, baadhi ya wafungwa waliomtaarifu ofisa usalama wa gereza hilo, Koplo Rashid kuhusu hali yake lakini inadaiwa akasema alikua anadanganya kuugua lakini usiku wa kuamkia jumanne alipoteza maisha.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, licha ya kukiri kutokea kwa kifo hicho, Kamishna Kiangae alikanusha kusababishwa na kipigo akisema mfungwa huyo alikua akiugua athma na malaria na habari za kupigwa hazina ukweli wowote.

Kamishna Kiange alisema mfungwa huyo amekua akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu na kabla ya kifo alizidiwa ghafla…..>>>Ni kweli kuna mfungwa amepoteza maisha lakini kifo chake hakihusiani na kupigwa alikua anaumwa athma na malaria na kwa muda mrefu amekua akiishi bila kufanya kazi kubwa

Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania leo July 06 2016

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 06 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments