Mix

Twitter imepunguza tena wafanyakazi… idadi ya watu waliopunguzwa ninayo hapa!

on

Twitter kwenye headlines mtu wangu, kama wewe ni mtumiaji mkubwa wa mtandao huo wa kijamii basi taarifa hii ikuguse popote pale ulipo…

CEO wa kampuni ya Twitter, Jack Dorsey ametangaza kupitia page yake ya Twitter kuwa kampuni hiyo imepunguza wafanyakazi 336 kwa nia na dhamira ya ‘kukuza na kubadilisha mfumo wao wa kutoa huduma zao kibiashara’, ambapo punguzo hilo la wafanyakazi ni sawa asilimia nane ya wafanyakazi wake 4100 waliopo kwenye branch mbalimbali za ofisi zao.

TWEET

Kwa mujibu wa mtandao wa AllHipHop, Twitter kupunguza wafanyakazi 336 itausaidia mtandao huo wa kijamii kupunguza na kubana matumizi ya hela licha ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kulipwa fidia yao… ukiacha hayo itawagharimu Twitter kiasi cha $ Milion 10 mpaka $ Milion 20 kurudisha biashara yao mstarini baada ya kufanya maamuzi haya.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments