Miezi kadhaa iliyopita kumekuwepo na mijadala mizito ya kisiasa na kitaifa juu ya upungufu wa chakula Tanzania. Taaarifa za upungufu wa chakula mwanzoni zilikataliwa na viongozi wa juu wa serikali lakini baadae walikiri kuwepo kwa tatizo hilo nchini.
Mwishoni mwa mwezi Januari 2017, Waziri wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba aliliambia bunge kwamba utafiti uliofanywa na Wizara kwa kushirikiana na wadau kadhaa, umegundua kwamba Wilaya 55 (kati 169 za Tanzania Bara na Visiwani) zilikumbwa na njaa.
Taarifa yake ilieleza kuwa tani 35,491 za nafaka zinahitajika kusambazwa kati ya mwezi wa pili na wa nne mwaka 2017 ili kukabiliana na upungufu huo uliowakumba watu 1,186,028”2 katika Wilaya hizo.
Leo March 1, 2017 Ripoti mpya ya taasisi ya utafiti ya Twaweza imetoa matokeo ya utafiti wake uliofanywa nchini ili kubaini ukweli wa suala la upungufu wa chakula.
Nimekuwekea hapa mambo nane yaliyobainika kwenye utafiti wa TWAWEZA.
Kaya nane kati ya kumi zimeripoti kwamba kipato chao hakikidhi mahitaji yao ya kila siku. #UpungufuChakula #Twaweza2017 pic.twitter.com/H9HLFUWcyU
— millardayo (@millardayo) March 1, 2017
Wananchi 9 kati ya 10 wanaona ni jukumu lao kuhakikisha wana fedha za kutosha ili kukidhi mahitaji ya kaya zao #UpungufuChakula #Twaweza2017 pic.twitter.com/2NnDNiytdz
— millardayo (@millardayo) March 1, 2017
Kpindi cha mwaka mmoja uliopita kaya moja kati ya 8 imepokea fao, faida au pesa kutoka ktk miradi ya serikali #UpungufuChakula #Twaweza2017 pic.twitter.com/YA4WqF4tlQ
— millardayo (@millardayo) March 1, 2017
Kaya 8 kati ya 10 (79%) zimeripoti kwamba zinahifadhi chakula kwa ajili ya dharura au kuepukana na njaa. #UpungufuChakula #Twaweza2017 pic.twitter.com/10LdXqHMrG
— millardayo (@millardayo) March 1, 2017
Kati ya waliohojiwa, 'Sauti za Wananchi' (78%) wanaripoti upungufu wa chakula katika maeneo wanayoishi #UpungufuChakula #Twaweza2017 pic.twitter.com/7ZhH6MyI0j
— millardayo (@millardayo) March 1, 2017
Kwa mujibu wa Benki Kuu mahindi yalipanda kutoka Tsh 400 Kilo 1 Jan 2015 hadi Tsh 852 kwa kilo kufika Dec 2016 #UpungufuChakula #Twaweza2017 pic.twitter.com/oKJyMOE5um
— millardayo (@millardayo) March 1, 2017
Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, kaya saba kati ya kumi zimepata hofu ya kupungukiwa na chakula #UpungufuChakula #Twaweza2017 pic.twitter.com/0jLhW6gWr4
— millardayo (@millardayo) March 1, 2017
September 2016, 45% waliripoti hofu ya kupungukiwa chakula, February 2017, idadi iliongezeka kufikia 65% #UpungufuChakula #Twaweza2017 pic.twitter.com/YoGdQd05aE
— millardayo (@millardayo) March 1, 2017
VIDEO: Ulipitwa na kilichoandikwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo March 1, 2017, Bonyeza play hapa chini kujua kila kitu