Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

DoneDEAL: Himid Mao kasaini ENNPI

on

Kiungo wa Timu ya taifa ya Tanzania Himid Mao baada ya timu yake aliyokuwa anaichezea ya Petrojet FC kushuka daraja kutokana na kumaliza nafasi ya 16 katika Ligi Kuu Misri inayoshirikisha timu 18, amepata dili katika club ya ENNPI.

Himid Mao amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu katika club ya ENNPI, club ambayo ilimaliza nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Misri msimu wa 2018/2019, haya yanaendelea kuwa mafanikio kwa Himid Mao ambaye alionesha kuaminiwa na Petrojet FC.

Pamoja na kucheza kwa kipindi kifupi katika timu hiyo Himid alionekana kuaminiwa na kucheza michezo 32 na kukosa michezo miwili pekee na kufunga magoli matatu, Himid Mao sasa ataendelea kukipiga Misri hadi 2022.

VIDEO: Kauli ya Kaseja baada ya kuichezea Taifa Stars baada ya miaka 6

Soma na hizi

Tupia Comments