Michezo

Club ya AS Roma imewafungia wachezaji wake kupiga picha na Drake

on

Club ya AS Roma ya Italia imefikia maamuzi ya kutangaza kuwafungia wachezaji wake kupiga picha na rapper wa Canada Drake hadi mwisho wa msimu 2018/2019, maamuzi hayo ya club hiyo yametangazwa kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa club hiyo ya AS Roma.

Layvin Kurzawa wa PSG akiwa na Drake.

Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni siku moja imepita toka staa wa club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Layvin Kurzawa kuonekana amepiga picha na Drake kabla ya mchezo ambao timu yake imepoteza kwa magoli 5-1 dhidi ya Lille.

Inaelezwa kuwa Layvin Kurzawa baada ya kupiga picha na Drake timu yake ndio ikaenda kupoteza mchezo wake wa pili Ligue 1 msimu huu, maamuzi hayo ya AS Roma yametoka kutokana na mastaa wengi wa soka ambao wamekuwa wakionekana wanapiga picha na Drake siku kadhaa kabla ya mchezo, basi game yao inayofuatia huwa wanapoteza.

Aubameyang na Drake

Pogba wa Man United na Drake.

Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?

Soma na hizi

Tupia Comments