Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

VIDEO: Rais wa TFF katua Nairobi kuongeza nguvu “Hakuna fitna iliyofanyika”

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya kuwasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Harambee Stars wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani 2020 zitakazofanyika nchini Cameroon, leo wamefanya mazoezi ya mwisho na Rais wa TFF Wallace Karia amewasili kuipa nguvu timu.

“Ni kweli sisi kwa dhamira yetu tumekuja kuhakikisha timu yetu inapita kesho, sidhani kwamba kuna fitna imefanyika hata timu yenyewe mahali iliopo hawakuitarajia tumejitahidi kuchukua tahadhari kama tulivyochukua Uganda, kwa hiyo tumechukua tahadhari zaidi ya zile za Uganda tulizochukua”>>> Rais wa TFF Wallace Karia

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa marudiano na Harambee Stars Jumapili ya August 4 2019, hiyo ni baada ya mchezo wao wa kwanza kumalizika kwa sare 0-0, Taifa Stars ili isonge mbele itahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kufungana magoli.

VIDEO: Mazoezi ya Mwisho ya Taifa Stars kabla ya kuivaa Kenya

Soma na hizi

Tupia Comments