Habari za Mastaa

Kutana na hii mpya ya Ty Dolla Sign ‘Saved’ feat E-40 – (Video)!

on

Wakati Album yake mpya Free TC ikiwa mtaani, rapper, producer na mtunzi wa nyimbo Ty Dolla Sign ameanza wiki kwa kusambaza love na ujio wa video yake mpya iliypewa jina ‘Saved’, ngoma iliyomshirikisha rapper E-40.

Single hii mpya imesimamiwa na Ty Dolla Sign mwenyewe kwenye uandishi, huku Mtayarishaji wa ngoma hii akiwa si mwengine bali DJ Mustard… Album mpya ya Ty Dolla Sign imebeba ngoma kadhaa zilizowashirikisha wakali wa HipHop na R&B Marekani, Kanye West, Kendrick Lamar, Wiz Khalifa, Future, R. Kelly na Trey Songz.

sign402

Lakini kama wewe ni shabiki wa Ty Dolla Sign basi ipokee hii popote pale ulipo, official music video ya Saved ipo hewani tayari na kama bado haijagusa macho yako basi feel free kuicheki ngoma hiyo hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments