Habari za Mastaa

Tyga anadaiwa Kodi? makosa ya kuvunja mkataba.. Ishu ya wizi je?

on

Headlines za Tyga kukwepa kulipa kodi sio kitu kipya kuhusu yeye, rapper huyo wa Cash Money Records anaonekana kutokujali sana kuhusu mashambulio hayo na wala hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi yake Kisheria!

Najua kuna watu wangu ambao ni mashabiki wakubwa wa rapper Tyga na pengine unajua au hujui kuwa Jimbo la California linamshitaki Tyga kwa malimbikizi ya kodi ya miaka mitatu, malimbikizi ya mwaka 2009, 2010 na mwaka 2011… Jimbo hilo linasema kuwa rapper huyo anadaiwa kiasi cha dola 19,124  ambazo ni sawa na Milioni 45 Tshs kwa pesa ya Kitanzania kwa miaka hiyo mitatu!

Tyga at the Exclusive Press Preview Of Tyga's Last Kings Flagship Store Featuring: Tyga Where: Los Angeles, California, United States When: 21 Feb 2014 Credit: revolutionpix/WENN.com

Tyga.

Hicho sio kitu pekee ambacho Jimbo la California linataka kutoka kwa rapper huyo, mwezi uliopita Mahakama iliamuru Tyga kumlipa mwenye nyumba wa nyumba aliyokuwa anaishi kodi ya nyumba ya miezi miwili ambacho kiasi chake kiligonga mpaka Milion 140 kwa pesa ya Kitanzania.

tyga6

Muonekano wa ndani wa duka la Tyga ‘Last Kings’.

Mengine ambayo Jimbo hilo linashitaki dhidi ya Rapper huyo wa Cash Money Records ni kesi ya kuvunja mkataba wake na moja ya club ya Las Vegas, mkataba ulikuwa wa dola 100,000 na ulikuwa unasema kwamba Tyga hatokuwa na mamlaka ya kuperform sehemu yoyote ile Las Vegas isipokuwa club ya ‘Body English’ jijini humo, Tyga alivunja mkataba huo ambao kwa shilingi ya Kitanzania tunazungumzia makubaliano yaliyozidi Milioni 200 kwa kwenda kutoa show kwenye club nyingine jijini Las Vegas!

Kwenye stori za Tyga kwenye headlines sasahivi zimeongezeka na hizo mtu wangu, ikiwemo kuvunja Mkataba na ishu za madeni.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments