Top Stories

Majibu ya saratani ya utumbo yawafanya wapenzi wafunge ndoa

on

Mwanamke mmoja Marekani ajulikanaye kwa jina la Katie Sutterby, 29, amefariki siku tatu tu baada ya kufunga ndoa kutokana na saratani ya utumbo.

Imeelezwa kwamba mwanadada huyu alipimwa na kukutwa na ugonjwa huo wiki tano zilizopita jambo lililopelekea mchumba wake Will Arnold aliyekuwa amepanga kumvalisha pete ya uchumba binti huyo mwishoni mwa mwaka huu kuamua kumchumbia binti huyo na kuanza mipango ya harusi.

Arnold, 38, alieleza kuwa kila kitu kilitokea haraka sana na daktari aliwaambia kuwa Katie kutokana na ugonjwa huo alikuwa amebakiza miezi michache tu ya kuishi kama sio mwaka mmoja hivyo ilibidi waandae harusi ili kumalizia siku hizo za Katie kama mume na mke na hata mpango wao wa kwenda Paris kwenye honeymoon haukufanikiwa kwasababu ya hali yake kiafya.

Ulipitwa na hii? “Nikimaliza mahusiano yangu na aliye South na kupata mwingine nitaweka wazi”-Diamond

 

Soma na hizi

Tupia Comments