Bondia Tyson Fury ameishangaza Dunia kwa kumpiga round ya 7 kwa TKO bondia Deontay Wilder katika pambano lililofanyika MGM Las Vegas Marekani na kutwaa Ubingwa Dunia WBC.
Wilder akimbizwa hospitali kwa kuumia sikio mara baada ya pambano huku akishindwa kuongea na waandishi wa habari kama ilivyokuwa imepangwa.
Bondia Tyson Fury kutokea Englanda walitoka sare katika pambano lao la kwanza ila hili la marudiano amefuta makosa yake na kuandika rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kumpiga Wilder kabla ya hapo hakuwahi kupoteza pambano.