Miezi kadhaa iliyopita tetesi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Tiwa Savage kuwa mapenzini na “Starboy” Wizkid hii ni kutokana na wawili hao kuwa pamoja sehemu mbalimbali hasahasa katika shows tofauti walizowahi kufanya pamoja.
Tiwa Savage kwenye mahojiano aliyofanya na radio ya Soundcity ameweka wazi kuhusiana na tetesi hizo za kuwa mapenzini na Wizkid na kusema kuwa “Nimeskia sana kuhusiana na tetesi hizo ila nimeamua kuzipuuzia”
“Kuna kipindi watu walisema niko kwenye mahusiano na Humblesmith, siku nyingine wakamtaja msanii mwingine, nitaendelea kuamini hizi habari mpaka lini? Nimekuwa kwenye muziki kwa muda kwahiyo baadhi ya vitu havinisumbui”
MKE WA MZEE MAJUTO: “HAKUNA WA KUNITOA, MALI TUMECHUMA WOTE”