Habari za Mastaa

Kila wiki Ty Dolla $ign atoa single mpya, wiki hii anaisogeza; ‘Sitting Pretty’ feat. Wiz Khalifa – (Audio)!

on

Rapper na Producer Ty Dolla $ign amekuwa akiziandika headlines za burudani kila mwisho wa wiki kwa kuachia single mpya kuelekea uzinduzi wa Album yake mpya Free TC, inayotegemea kuwa sokoni Tarehe 13 November 2015… wiki hii je?

Baada ya kuziandika headlines ijumaa iliyopita kwa kuachia video mpya, ‘Solid’ alioshirikiana na msanii mkongwe wa R&B Marekani, Baby Face… wiki hii Ty Dolla $ign amerudi na single mpya ambayo ndani mkali mwengine wa HipHop, Wiz Khalifa kashirikishwa.

TYWIZ2

Ty Dolla $ign.

Wimbo unaitwa ‘Sitting Pretty’, na single hii ni miongoni wa nyimbo zinazobeba Album mpya ya Ty Dolla $ign Free TC. Wasanii wengine watakaosikika kwenye Album mpya ya msani huyo ni pamoja na Kanye West, Kendrick Lamar, Brandy, Trey Songz, P Diddy, R. Kelly, Future na wengine kibao!

Hapa chini nimeisogeza kwako single mpya ya Ty Dolla $ign, bonyeza play kuisikiliza.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments