AyoTV

“Hatuombi watu kuacha uhalifu, tunawaambia tutapambana nao” – Mwigulu

on

Usalama wa Kibiti ambako kumekuwa kukiripotiwa mauaji ya viongozi wa vyama na serikali na raia imeelezwa kuwa ni salama tofauti na kipindi cha nyuma ingawa bado Jeshi la Polisi litaendelea kuhakikisha kila anayejihusisha na uhalifu anatiwa katika mikono ya sheria popote alipo.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba amesema kuwa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo mauaji ya raia yaliripotiwa kila mara lakini sasa hali imekuwa shwari:>>>”Kipindi kilichopita ilikuwa kila baada ya siku mbili unasikia kuna tukio lakini sasa utaona kwamba kwa muda haujasikia matukio ya aina hiyo.

“Sisi kwenye mambo ya uhalifu hatuwaombi watu kuacha. Hatuwabemebelezi watu kuacha uhalifu. Tunawaambia tutapambana na uhalifu na tutapambana na wahalifu mmoja baada ya mwingine. Tutapambana nao na tutahakikisha kwamba tunakomesha uhalifu.” – Waziri Mwigulu Nchemba.

VIDEO: “Usipofanya kazi hautokula na usipokula utakufa, lazima niwaambie ukweli” – RAIS MAGUFULI…full video bonyeza play hapa chini kuitazama!

Kitu Zitto Kabwe ameongea mbele ya Rais Magufuli Kigoma…tazama kwenye video hii chini.

Soma na hizi

Tupia Comments