Michezo

Juma Luzio na Mzamiru wameipatia Simba point tatu dhidi ya Taifa Jang’ombe

on

Baada ya kuchezwa mchezo wa pili wa Kundi wa Kombe la Mapinduzi 2017 leo January 1, usiku wa January 1 ilikuwa ni zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi A dhidi ya Taifa Jang’ombe katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

Huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba lakini ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Taifa Jang’ombe ambao mchezo wao wa awali walicheza dhidi ya Jang’ombe Boys na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Hassan Seif.

img-20170101-wa0087

Taifa Jang’ombe leo wamekubali kupoteza mchezo dhidi ya Simba kwa goli 2-1, magoli ya Simba yakifungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 28 na Juma Luzio dakika ya 42, lakini beki wa Simba Novaty Lufungo akijifunga dakika ya 76 baada ya Taifa Jang’ombe kupiga kona iliyosababisha goli hilo.

img-20170101-wa0086

Msimamo wa Kundi A kwa utakuwa unaongozwa na URA wenye point tatu na magoli mawili wakifuatiwa na Simba wenye point tatu sawa Taifa Jang’ombe aliyepo nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, Simba watarudi uwanjani January 3 saa 2:30 usiku kucheza dhidi ya KVZ.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments