Mix

Habari kubwa 6 kwenye Tv za Tanzania April 27 2017

on

Hii ni kwa wale watu wangu wanaopenda kufuatilia habari kupitia Tv za Tanzania na Usiku wa leo April 27 2017 tayari nimekukusanyia habari sita kubwa ambazo zimeruka kwenye taarifa ya habari usiku huu na nisingependa ikupite hata moja.

Habari ya Azam Two – Riport ya Spika Bungeni juu ya mauwaji wa askari 8

Spika wa Bunge Job Ndugai amekabidhi serikalini riport ya kamati ya mambo ya nje ulinzi na Usalama iliyopokea undani juu ya mauwaji ya askari nane walio uwawa katika shambulio la kushtukiza huko Kibiti mkoani Pwani ambapo amekabidhi ripoti hiyo ili serikali ifanyie kazi mapendekezo yaliyowasilishwa Bungeni na kamati ambayo iliweza kumuhoji waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nnchemba.

Clouds Tv Habari – Kiama cha wenye Vyeti Feki

Rais wa jamuhuri ya Muungano waTanzania John Pombe Magufuli kesho tarehe 28 2017 atapokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wauma katika ukumbi wa Chimwaga mkoa wa Dodoma na taarifa hiyo itawasilishwa kwa Rais na waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki.

Habari ya Star Tv – Mauwaji Tarime 

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Richard Ndonge mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa mtaa wa kehogoma katika wilaya ya Tarime mkoani mara ameuwawa na watu wasiojulikana na mwiliwake kutubwa katika bwawa la maji lililopo katika kitongoji cha kimusi huko Tarime.

Habari ya Chanel 10 – Himaya ya Umoja wa Forodha (EAC) kuanza rasmi julai 31 

Nchi sita wanachama wa jumiya ya Afrika mashariki zimekubaliana kwa pamoja kuanza utekelezaji wa matumizi ya mfumo wa himaya ya moja ya forodha ifikapo julai 31 mwaka huu kwa madhumuni ya kuongeza kasi ya mzunguko wabidhaa pamoja na kupunguza garama za kufanya biashara ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki.

Habari ya Chanel 10 – Tishio la silaa za Nyuklia

Rais Donald Trump amewaeleza Maseneta wote 100 wa bunge la taifa hilo kuhusu tishio la korea ya kaskazini na kubaini mikakati ya kushinikiza nkubaini mikakati ya kiuchumi na ya kidipromasia huku mpango ni kuishinikiza Korea ya kaskazini kusitisha mpango wa makombora ya masafa marefu ya nuklia.

Habari ya Azam Two – Odinga Uso kwa Uso tena na Kenyatta

Muungano wa Vyama vya Upinzani nchi Kenya NASA umemtangaza mwanasiasa mkongwe nchini humo Raila Odinga kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa nchini kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika August 8 2017 huku Kalonzo Musokya akitangazwa kuwa mgombea-mwenza.

 

VIDEO: Maswali na majibu yaliyosikika Bungeni April 27, 2017

Soma na hizi

Tupia Comments