Habari za Mastaa

U HEARD: “Mimi sina mpenzi, Young Dee siyo mpenzi wangu” – Mamisa

on

U-heard ya April 13 2017 kwenye XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametukutanisha na stori inayomhusu rapa Young Dee kuonekana akiwa na Gigy Money kwenye video inayosambaa mitandaoni ikidaiwa kumuumiza mwanamke aliyezaa naye, Mamisa.

Soudy Brown alipiga story na Young Dee kujua ukweli kuhusu video hiyo na majibu yake yalikuwa haya…>>>“Nilikuta watu wana mzuka na mimi nikajichanganya kucheza, so, kama kuna mtu alishoot mimi sijui chochote. Amber Lulu ni msanii tu halafu ni mtu ambaye sijawahi hata kukaa naye.” – Young Dee.

Alipoulizwa Mamisa kuhusu video hiyo alisema:...>>>”Mimi sina mapenzi na mtu, Young Dee siyo mpenzi wangu. Huwezi kuwa na mtu ambaye haeleweki maana kuna vitendo mtu anaweza kufanya vikawa vinakuumiza. Mimi nipo kwao na naishi kwao ila kuna vitu vingine vinaumiza na mimi ndio najua uchungu wa mtu.

“Mimi sijamkataza Young Dee kuwa na mtu ila muda mwingine unatakiwa mtu ujielewe, siyo unamuonesha mtu hadharani halafu wakati mwingine unamwambia anatukana. Hebu imagine, ungekuwa wewe ungefanyaje?” – Mamisa

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza…

VIDEO: Safari ya kwanza kwa ‘Navy Kenzo’ Israel wameyaongea haya

VIDEO: Navy Kenzo wamewasili Israel kwa ajili ya show yao

Soma na hizi

Tupia Comments