Habari za Mastaa

U HEARD: Chege aizungumzia picha waliyopiga na Juma Nature

on

U Heard ya Clouds FM leo November ipo na stori kuhusu picha iliyosambaa kuanzia weekend iliyopita wakati wa kilele cha msimu wa FIESTA 2016 ikiwaonesha Juma Nature na Chegge wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakidaiwa kuwa walikuwa hawana maelewano mazuri yaani beef ya chini chini.

Mtangazaji Soudy Brown amepiga story na Chege Chigunda kutoka TMK Wanaume Family ili kufahamu kama kuna ukweli wa kile kinachoelezwa kuwa yeye na Juma Nature wamekuwa kwenye stori za kutokuwa sawa kama zamani kwamba wana beef ya chini chini na sababu kubwa ikidaiwa ni mwanamke.

>>>’Kwanini watu washangae hiyo picha hii sio mara ya kwanza mbona tumepiga picha na wasanii wengi, tulikuwa sehemu moja tumekutana tunafurahi, mimi sina beef na mtu yeyote, najua nilichofanya ni kupiga picha hakuna beef’ – Chege

Full Stori iko hapa, Bonyeza play kusikiliza.

 

VIDEO: Kocha Lwandamina kutoka Zesco ya Zambia amelizungumzia Sola la Tanzania, Bonyeza play.

Soma na hizi

Tupia Comments