Habari za Mastaa

U HEARD: Mapenzi ya Harmonize na Wolper yadaiwa kuvunjika

on

Taarifa zinazosambaa na ku-make headlines katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni kuhusu mahusiano baina ya staa wa Bongo Fleva Harmonize na staa wa Bongo movie Jackline Wolper ambao unadaiwa kuvunjika.

Kupitia U-heard ya XXL ya Clouds FM leo April 21, 2017 mtangazaji Soudy Brown ametuletea stori hiyo ambapo inadaiwa kuwa Harmonize yupo mapenzini na mwanamke mwingine wa kizungu ambaye inasemekana kuwa tayari ana ujauzito wa staa huyo wa Matatizo.

Baada ya Soudy kuwatafuta wawili hao na kuwakosa alimtafuta mmoja wa mameneja wa WCB Babu Tale ili kujua ukweli kuhusu hili na majibu yake yakawa haya>>>”Tuzungumze biashara ya Chibu Perfume leo. Utakapompata Harmonize utazungumzia hilo. Mimi sio manager wa mapenzi ya wasanii wangu, namanage biashara na kazi zao basi.” – Babu Tale.

Bonyeza Play kusikiliza Full story hapa chini…

VIDEO: Harmonize na Rich Mavoko walivyoitambulisha ‘Show Me’ Mbagala

Soma na hizi

Tupia Comments