AyoTV

Maneno ya Sumaye kuhusu Katiba, kuzuiliwa kwa mikutano ya kisiasa (+Video)

on

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (CC) ya CHADEMA Frederick Sumaye leo July 14, 2017 amebainisha kuwa kitendo cha kuzuiwa kwa mikutano ya siasa kunayumbisha demokrasia.

Sumaye amesema kuwa demokrasia ya vyama vingi vya siasa ni ushindani wa kisiasa huku akiweka wazi kuwa licha ya kuhitajika kwa utawala bora na demokrasia, bado inahitajika Katiba ambayo itatoa Tume huru ya Uchaguzi.

>>>”Tunaitaka Katiba ambayo itatoa Uhuru kwa vyama vyote vya siasa, kuweka utaratibu mzuri wa uchaguzi kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi. Tume huru namaanisha Tume huru, siyo Tume ambayo imebandikwa bandikwa.

“Demokrasia ya vyama vingi unaweza ukawa nayo lakini usiwe na mfumo sahihi wa demokrasia. Mfumo sahihi ni pale ambapo watu wote wanatii Katiba, wanatii Sheria, vyama vyote vinafanya kazi kwa uhuru. Hakuna chama kinanyimwa haki ya kufanya shughuli zake.” – Frederick Sumaye.

Rugemalira, Sethi wamefikishwa tena Kisutu leo, maamuzi ya Mahakama je?

Soma na hizi

Tupia Comments