Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo ikishirikiana na Jeshi la Polisi limemkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kwa utapeli na kujipatia fedha kutoka kwa wanafunzi wa Taasisi kwa ahadi ya kuwasaidia katika ufaulu wao.
Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Zakayo Lukumay amesema wimbi la utapeli ndani ya Taasisi hiyo limeshika kasi siku za hivi karibuni ambapo kikundi cha watu wasiojulikana kimekua kikiwarubuni wanafunzi na kuwaibia fedha.
Watu hao wameelezwa kutumia jina la Taasisi hiyo na kuwaahidi wanafunzi kuwa wanaweza kuwasaidia kufaulu mitihani yao endapo watawapatia pesa ambapo hadi sasa tayari mtu mmoja ameshakamatwa na Polisi na upelelezi unaendelea ili kujua kama wapo watu wengine wanaohusika ili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
BREAKING: Serikali imekichukua kiwanda cha Ngozi Africa Tanneries, Mwanza…tazama kwenye video hii hapa chini!!!
Uliikosa hii? Tajiri namba 1 wa dunia Bill Gates yuko Tanzania