Michezo

Yanga SC bado ni wababe tu wa Azam FC

on

Rekodi imeendelea kuibeba club ya Yanga SC dhidi ya Azam FC wakiwa wanaingia uwanjani kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019, game hiyo ilichezwa katika uwanja wa  Uhuru Dar es Salaam uliyowekewa nyasi mpya za bandia na Yanga kuwa timu ya kwanza kuanza vizuri katika uwanja huo.

Yanga leo ikiwa katika mchezo huo wa ugenini imefanikiwa kuondoka na point tatu baada ya ushindi wa goli 1-0, lilifungwa na Mrisho Khalfan Ngassa aliyetumia vyema pasi safi ya Ibrahim Ajibu, ushindi huo unakuwa ni ushindi wa 8 wa Yanga dhidi ya Azam FC wakiwa wamewahi kukutana mara 21, sare zikiwa 7 na Yanga amepoteza mara sita tu dhidi ya Azam.

Matokeo hayo yanawafanya Yanga waendelee kuongeza Ligi kwa kuwa na jumla ya point 77 wakiwa wamecheza michezo 33, wakifuatiwa na Simba SC wenye point 69 wakicheza michezo 27 na wana viporo michezo 6, Azam FC wao wameendelea kuwa nafasi ya tatu wakiwa na point 66 walizovuna katika michezo 33.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments