Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Hii ndio ilikuwa ahadi ya Jonas Mkude kwa Manara kabla kuingia robo fainali

on

Club ya Simba SC kuelekea mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya TP Mazembe ya Congo DRC, leo afisa habari wao ameongea mambo mbalimbali kuhusiana na mchezo huo sambamba na kutangaza viingilio vya mchezo huo.

Viingilio uongozi wa Simba SC umeweka kiasi cha chini zaidi ni kuanzia Tsh 4000, Tsh 10000, Tsh 20000 na Tsh 100000 kwa VIP Platnum, hii ikiwa ni huduma mpya ya utaratibu wa Simba kwa wale mashabiki watakaokata tiketi za gharama hiyo watapelekwa na gari binafsi hadi uwanjani.

Hata hivyo Haji Manara ameeleza kuwa Simba SC kuifunga Mazembe inawezekana ukizingatia Jonas Mkude, aliwahi kumwambia kuwa muda mchache kabla ya game ya Simba vs AS Vita jijini Dar es Salaam, kuanza alimwambia kuwa kama wakipita basi hatua inayofuata watawashangaza watu.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments