AyoTV

Dismas Ten ameizungumzia hasara ya Tsh Milioni 16.5 ya Yanga kujitakia

on

Club ya Dar es Salaam Young Africans jana kutoka Shirikisho la soka Tanzania TFF ilitangazwa kupigwa faini ya Tsh milioni 3 kwa kosa la kutumia mlango usiokuwa rasmi kuingilia uwanjani April 4 2019 katika mchezo dhidi ya Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara.

Yanga ambayo kwa sasa ipo katika hali mbaya kiuchumi imeingia jumla ya hasara ya Tsh Milioni 16.5 ndani ya siku 17, hasara ambayo baadhi ya watu wanadai kuwa ni yakujitakia kwa sababu inaepukika.

Toka February 16 hadi April 4 2019 Yanga imetenda jumla ya makosa kama matano yanayojirudia rudia na kuisababishia club hiyo iliyopo katika hali mbaya kiuchumi kuingia hasara ya Tsh milioni 16.5 kutokana na kupigwa faini na TFF.

Baadhi ya makosa ambayo Yanga imetenda ni kutoingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi na kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko a wakati wa ukaguzi katika michezo dhidi ya JKT Tanzania February 10, Simba SC February 16, KMC March 10 na April 4 dhidi ya Ndanda FC

Amplifaya ya Clouds FM imempata afisa habari wa Yanga SC Dismas Ten na kumuuliza kuhusiana na ishu hiyo? kwa nini wamekuwa wakitenda makosa ya aina moja kwa kujirudia rudia wakiwa wanajua wanaingiza club yao katika hasara inayoepukika.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments