Habari za Mastaa

Rihanna atajwa na Forbes kuwa msanii wa kike tajiri zaidi duniani

on

Kwa mujibu wa jarida la Forbes limemtaja Rihanna kuwa mwimbaji wa kike tajiri zaidi duniani,  utajiri wa msanii huyo umetajwa kufikia dola Million 600 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh Trilioni 1.3 ikielezwa utajiri huo pia umetokana  na bidhaa za Brand yake ya Fenty Beauty.

Inaelezwa kuwa superstar huyo mwenye umri wa miaka 31 ameingiza pesa nyingi nje ya mapato ya muziki ikiwa pamoja na brand yake ya urembo Fenty Beauty ambayo inafanya vizuri sokoni kwa sasa na kutajwa kumuingizia thamani ya dola milioni 100 sawa na zaidi ya Tsh Bilioni 230.

Ukizungumzia ndani ya uwanja wa muziki kazi ya mwisho ya Rihanna ilikuwa ni Album yake ya ‘ANTI’ aliyoiachia mwaka 2016, katika list hiyo mpya ya forbes imewataja waimbaji wanaomfuatia Rihanna ni pamoja na Madonna mwenye utajiri wa dola milioni 570, Celine Dion dola milioni 450, Beyonce dola milioni 400.

VIDEO: A-Z: SIRI YA MONALISA KUPATA ‘MASHAVU’ YA UBALOZI HII HAPA, MWENYEWE AFUNGUKA

Soma na hizi

Tupia Comments