Habari za Mastaa

‘Fall’ ya Davido inashikilia rekodi ndani ya chart za Billboard Marekani

By

on

Davido anaendelea tena kushika headlines na hii ni baada ya wimbo wake wa ‘Fall’ aliouachia rasmi June 2,2017 kuweka rekodi kwenye chart za Billboard nchini Marekani.

Wimbo huo wa Davido umetajwa kuwa wimbo wa kwanza kutoka kwa msanii wa Nigeria kukaa muda mrefu zaidi kwenye chart hizo za Billboard ukilinganisha na nyimbo nyingine za Afrobeats ambazo ziliwahi kukaa kwenye chart hizo.

Wimbo wa ‘Fall’ unashikilia nafasi ya 23 katika kipengele cha ‘Billboard R&B/HipHop Airplay” ikiwa wimbo huo umekaa wiki nne mfululizo.

On Air: Historia, Wazazi wa Nandy walivyompeleka Nandy kwa Mganga

Soma na hizi

Tupia Comments