Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Naibu Waziri Juliana Shonza atoa onyo kwa Gigy Money “atavunjika shingo”

on

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza ameitumia kauli iliyotolewa na Rais Magufuli siku kadhaa zilizopita kuhusiana na wale wanaotumia mitandao ya kijamii kumong’onyoa maadili ya Tanzania wachukuliwa hatua.

Hivyo Naibu Waziri Juliana Shonza ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpa onyo msanii wa Bongo Fleva Gigy Money pamoja na wengine ambao wanatumia mitandao ya kijamii vibaya na kuvunja maadili ya Tanzania na kuwaambia kuwa huenda wamepata ujumbe wao.

Walengwa natumai ujumbe wenu mmeishaupata kina @gigy_money_og na wenzio, msidhani hatuwaoni , “ashupazaye shingo yake atavunjika na wala hatapata dawa”. – Juliana Shonza

ARISTOTE: MASTAA WATANO WANAOVAA NYWELE ZA GHARAMA BONGO

 

Soma na hizi

Tupia Comments