Michezo

PSG kumshitaki staa wa zamani wa Man United Patrice Evra

on

Club ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa imepanga kumshitaki beki wa zamani wa Man United Patrice Evra kutokana na kutoa lugha ya kebehi na kuwadharau wa wachezaji wa PSG baada ya kutolewa na Man United katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

PSG inapanga kumshitaki mchezaji huyo kutokana na kauli yake ya kueleza kwa kejeli kuwa wachezaji wa PSG hawana **** kiu** kitu ambacho uongozi wa PSG umekitafsiri kama dharau kubwa na kauli ya kuwavunjia heshima wachezaji wao ambao wamekuwa wakiipambania club.

Man United iliitoa PSG katika michuano ya CAF Champions League licha ya kupoteza mchezo wa kwanza Old Trafford kwa 2-0, game ya marudiano ilibadilika na kujikuta PSG wakipoteza mchezo huo nyumbani kwao kufungwa kwa magoli 3-1, (agg 3-3), kama humkumbuki Patrice Evra aliwahi kuichezea Man United kwa miaka 8 (2006-2014) na kujiunga na Juventus.

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments