Michezo

AFCON 2019 VAR itatumika kama World Cup 2018 ilivyokuwa

on

Baada ya kumalizika kwa michezo ya kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika 2019 (AFCON 2019) zitakazofanyika nchini Misri, kuelekea michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi kuanzia June 19 2019, kwa mara ya kwanza mwaka huu ndio itatumika VAR.

Shirikisho la soka Afrika CAF limeweka wazi kuwa kuanzia hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON 2019, wataanza kutumia teknolojia ya video za usaidizi kwa waamuzi VAR (Video Assista Referee) katika kutolea maamuzi katika game zote za 16 bora.

Pamoja na kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakiipinga teknolojia hiyo kuwa inapoozesha mchezo wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika Urusi, imeonekana kuzidi kutawala baada ya kuona inatumika katika AFCON na hata baadhi ya Ligi wameonesha kuikubali, droo ya kupanga makundi ya michuano ya AFCON 2019 itachezeshwa April 12 2019 Cairo Misri.

MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS

Soma na hizi

Tupia Comments