Michezo

Patrick Aussems na John Bocco wameng’aa TPL mwezi March

on

Leo Jumatano ya April 3 2019 kocha mkuu wa club ya Simba SC Patrick Aussems na mchezaji wake John Bocco kuwa ndio washindi wa tuzo za mwezi March za Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019.

Kocha wa Simba Patrick Aussems ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya kocha bora wa mwezi March wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019, huku mshambuliaji wa timu hiyo John Bocco akitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi March.

John Bocco amewashinda Donald Ngoma wa Azam FC na Jaffari Kibaya wa Mtibwa Sugar waliokuwa wanawania tuzo hiyo, ndani ya mwezi March Aussems ameiongoza Simba SC kucheza michezo mitatu ya Ligi Kuu na kushinda michezo yote, wote Aussems na Bocco watapewa tuzo na zawadi ya pesa ya Tsh Milioni 1 kila mmoja.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments