Michezo

Louis van Gaal hatimae amejibu tuhuma za Di Maria dhidi yake

on

Kocha wa zamani wa club ya Man United Louis van Gaal aliyeamua kustaafu jumla kazi ya kufundisha soka toka afukuzwe kazi Man United kwa sababu za kiwango cha timu hiyo kutowaridhisha mabosi wa Man United, amejibu shutuma dhidi yake zilizotolewa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Angel Di Maria.

Di Maria ambaye hakuwa na mahusiano mazuri na Louis van Gaal na baadae kuondoka kutimkia club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, alidai kuwa Louis van Gaal ndio alisababisha kuhama Man United na kujiunga na PSG, Kwani Louis van Gaal alikuwa haoneshi kumkubali na ndicho kilichofanya hata hasirudi Man United wakati wa maandalizi ya msimu hadi ana hama.

Akihojiwa na BBC Van Gaal amejibu yote na kueleza tofauti ya Mourinho na Solskjaer “tofauti kubwa kati ya Jose Mourinho na Solskjaer ni kuwa Solskjaer anapata matokeo ila namna Man United ya sasa inavyocheza sio sawa na ilivyokuwa inacheza wakati wa Ferguson, Di Maria anasema mimi ndio nilikuwa tatizo? nilimpanga katika nafasi zote za ushambuliaji lakini hakunishawishi katika nafasi zote hizo hakuweza kukabiliana na mfululizo wa presha ya EPL”

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments