Michezo

Watakaotinga fainali ya Coppa Italia kujulikana leo na kesho April 25 2019

on

Vigogo wa Serie A club ya Juventus wameimiliki Coppa Italia kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni na wameshinda mara nne mfululizo hadi msimu uliopita, lakini baada ya kutolewa na Atalanta kwenye robo fainali, jina la Juventus halitaandikwa kwenye Kombe la Coppa Italia baada ya mchezo wa fainali May 15 2019.

Usiku wa leo na kesho michezo ya pili ya nusu fainali itapigwa, timu zote zina nafasi baada ya michezo ya kwanza yote kuisha kwa sare, Lazio mara ya mwisho wameshinda taji hilo mwaka 2013, katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali walilazimishwa suluhu nyumbani dhidi ya AC Milan. Club hiyo ya jijini Rome imekuwa na matokeo dhaifu hata kwenye ligi msimu huu.

Lakini ili kufanikisha hilo wanahitaji kuwafunga Milan walau goli moja usiku wa leo, ambapo wenyeji wao wamekuwa wagumu sana kuruhusu magoli, golikipa wa timu ya taifa ya Italia Gianluigi Donnarumma na Pepe Reina – ambao wameshirikiana kulinda lango la Milan bado hawajaruhusu bao hata moja kwenye Coppa Italia, hii itawaongezea presha washambuliaji wa Lazio.

Lazio wanatakiwa kufikiria namna ya kumzuia mshambuliaji wa AC Milan Krzysztof Piątek, ambaye anaongoza kwa magoli kwenye michuano hiyo akiwa na jumla ya mabao nane hadi sasa, Kama mashabiki waliotazama mechi ya kwanza ya Lazio na Milan walinyimwa burudani ya magoli basi mchezo wa Fiorentina na Atalanta uliwapa burudani yote, timu hizo zilifungana jumla ya magoli sita. Aisee!!

Fiorentina na Atalanta wote wana muda mrefu sana hawajashinda taji hilo, Fiorentina mara ya mwisho wameshinda mwaka 2001 wakati Atalanta wameshinda mara moja tu na ilikuwa mwaka 1963, Atalanta ambao bado wanagombania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao watakuwa na mchezo mwingine mwisho wa wiki, Game ya AC Milan na Lazio ni leo usiku na Atlanta na Fiorentina kesho April 25 kupitia ST World Football

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

 

Soma na hizi

Tupia Comments