Michezo

Katika maisha ya Jurgen Klopp Man United ndio wamewahi kumshangaza zaidi

on

Pamoja na kuwa mchezo wa marudiano wa UEFA Champions League wa hatua ya 16 bora kati ya PSG dhidi ya Man United kuwa gumzo kwa penati ya dakika za mwisho, wengi wameshangazwa na uwezo wa Man United kwenda kupindua matokeo ugenini.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Old Trafford ambao ni uwanja wa nyumbani wa Man United walishuhudiwa Man United wakipoteza kwa magoli 2-0, hivyo baada ya kwenda ugenini jijini Paris na Man United wakashinda kwa magoli 3-1(agg 3-3)  na kuitoa PSG ni wengi walishangazwa na matokeo hayo.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ni moja kati ya watu walioshangazwa na leo ameweka wazi hisia zake hizo akihojiwa na Canal Football kwa kusema kuwa huo ni mchezo ambao wa timu isio kuwa na bahati aliwahi kuuangalia katika maisha yake kwa maana PSG walitawala mchezo game zote mbili.

“Moja kati ya michezo iliyokosa bahati ambayo nimewahi kuiangalia ni (PSG vs Man United) kiukweli, niliiangalia ile game na kusema wow, kiuhalisia ilikuwa haiwezekani (PSG) kupoteza walikuwa wazuri katika michezo yote miwili (ugenini na nyumbani”>>> Jurgen Klopp

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments