Habari za Mastaa

Mwili wa Michael Jackson kufukuliwa kwa ajili ya uchunguzi

on

Kwa mujibu wa mtandao wa Radar Online unaripoti kuwa mwili wa Mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson unaweza kufukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi kufuatia tuhuma za ulawiti zilizotolewa na wavulana tofauti hivi karibuni.

Kupitia makala ya ‘Leaving Neverland’ imebaini kuwa Mfalme huyo wa Pop aliwahi kuwalawiti wavulana zaidi ya 30 wakiwa na umri mdogo huku waathirika 11 tayari wamejitokeza na kukiri unyanyasaji huo na kusema kuwa MJ alifanya kitendo hicho wakiwa na umri kati ya miaka 7 mpaka 14.

Inaripotiwa kuwa mmoja wa mashuhuda aliuambia mtandao huo kuwa MJ alikuwa akiwaliti watoto wengi kutokana na wao kwenda kumtembelea nyumbani kwake na alikua akifanya hivyo hasa kwa walemavu pamoja na wagonjwa waliokuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Kutokana na tuhuma hizo mwili wa Marehemu MJ utafukuliwa kwaajili ya vipimo vya DNA kwenye mabaki ya sehemu za mwili wake ili kuthibitisha ukweli unaosemwa. Mwaka 1993 MJ aliwahi kufunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mvulana mwenye umri wa miaka 13.

LIVE: Ziara ya Wasanii Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa DSM kuitazama reli ya kisasa

Soma na hizi

Tupia Comments