Michezo

TFF imewaondoa waamuzi waliochezesha game ya KMC vs Simba April 25 2019

on

Shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza kuwaondoa katika orodha ya waamuzi watakaochezesha michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu, TFF imetangaza kuwaondoa waaamuzi Abdallah Kambuzi, Godfrey Masakila na Consolata Lazaro.

Waamuzi hao waliyoondolewa ni wale waliochezesha mchezo wa KMC dhidi ya Simba SC April 25 2019 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, uamuzi huo umefikiwa baada ya TFF kuridhisha kuwa waamuzi hao hawajaonesha kiwango cha kuridhisha katika mchezo huo.

Katika mchezo huo Kambuzi alikuwa ni muamizi wa katikati akisaidiana na  Gofrey Masakila na muamuzi msaidizi namba 2 Consolata Lazaro, pamoja na hayo TFF inawaonya waamuzi kuwa makini na uchezeshaji wa mechi za TPL kwa kuzingatia sheria 17 za soka.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments