Michezo

Patrice Evra adai Pogba atachoka na msimu huu anaweza kuondoka

on

Beki wa zamani wa Man United Patrice Evra ameweka wazi kuwa rafiki yake ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa na club ya Man United Paul Pogba, ataondoka ndani ya club hiyo mwisho wa msimu wa 2018/2019 kutokana na kudaiwa kuwa kutopendwa na mashabiki wa Man United na kumuandama kwa maneno.

“(Pogba) ana magoli mengi ana pasi nyingi za magoli najua unaweza ukauliza kuhusiana na uongozi wake lakini katika mechi chache zilizopita ulikuwa ulikuwa unataka sana kutoka kwake, hivyo unaweza ukamkosoa kwa sasa lakini kiujumla ni mchezaji bora msimu huu” >>> Patrice Evra

“Ni kwa sababu tu yeye ni Pogba, anaweka style za nywele, anapenda kucheza na kuweka katika instagram yake kila kitu, watu wataanza kumkosoa na kusahahu kila kitu namna alivyokuwa mchezaji, ni yeye (Pogba) na David (De Gea) ndio wanaweza kucheza timu kubwa Ulaya”>>>Patrice Evra

Patrice Evra ambaye amewahi kucheza Man United na timu ya taifa ya Ufaransa ni rafiki wa Paul Pogba ambaye ni mfaransa mwenzake, hivyo kauli yake inadaiwa kuwa na mashiko kuwa kuna uwezekano ikawa ina nguvu staa huyo ataondoka kutokana na maneno ya kumuandama kuwa mengi.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments