Michezo

Vincent Kompany anaondoka Man City kwenda kuwa kocha mchezaji

on

Nahodha wa Man City ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya Ubelgiji Vincent Kompany ametangaza kuwa anaondola Man City na kuamua kurejea nyumbani kwao Ubelgiji, ambapo ndiko alikozaliwa na kukulia.

Kompany anaondoka Man City baada ya kudumu kwa miaka 11 ila ameamua kurudi nyumbani kwao wakati huu akiwa na umri wa miaka 33, hivyo anarudi katika club yake iliyomlea ya Anderlecht akiwa na jukumu la kwenda kuwa kocha mchezaji.

Kwa taarifa hizo ni wazi Kompany anaenda kuandaliwa kuwa kocha wa club ya Anderlecht,  Kompany anaondoka Man City akiwa kaichezea jumla ya michezo 360, akifunga magoli 20, mataji 4 ya EPL, League Cup 4, FA Cup 2 na Ngao ya Jamii 2.

Kompany alianzia soka lake katika Academy ya Anderlecht akiwa na umri wa miaka 14 2000 na 2003 akapandishwa timu ya wakubwa ya Anderlecht na kucheza kwa misimu mitatu, 2006 akajiunga na club ya Humberger SV aliyodumu nayo kwa misimu miwili na kwenda Man City 2008.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments