Habari za Mastaa

Ben Pol kaweka wazi thamani ya pete aliyomvisha Anerlisa

on

Baada ya watanzania waliowengi wakitaka kufahamu zaidi kuhusiana na penzi la msanii wa Bongo Fleva Ben Pol na mpenzi wake raia wa Kenya Anerlisa wanaendeleaje katika mahusiano yao baada ya hivi karibuni kuonekana sehemu tofauti tofauti pamoja, kuchumbiana na mipango yao ya sasa.

Ben Pol kupitia Youtube Channel yake ameeleza mengi tusio yafahamu kuhusiana na mpenzi wake Anerlisa, Ben Pol amekanusha taarifa za Anerlisa kuwa mjamzito na kueleza kuwa alichokipost kilikuwa ni ndoto tu kuwa anatamani kuwa na watoto mapacha.

Kuhusu kumvisha pete ni kweli Ben Pol amekiri kukusudia kuingia nae katika ndoa na kuanza familia nae, ndio maana ameamua kuwa serious na kumvisha pete ya dola 11000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 22, Ben Pol amesisitiza kuwa mahusiano yake na Anerlisa ni upendo tao tu ndio unawaunganisha na sio pesa.

VIDEO: A-Z: SIRI YA MONALISA KUPATA ‘MASHAVU’ YA UBALOZI HII HAPA, MWENYEWE AFUNGUKA

Soma na hizi

Tupia Comments