Premier Bet SwahiliFlix Ad Vodacom Ad

Habari za Mastaa

Mwimbaji Oliver Mtukudzi afariki dunia leo Zimbabwe

on

Muimbaji mkongwe kutokea Zimbabwe Oliver Mtukudzi amefariki dunia leo January 22,2019 katika hospitali ya Avenues Clinic iliyopo Harare, Zimbabwe baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Oliver Mtukudzi amefariki akiwa na umri wa miaka 66 na ameacha jumla ya watoto wa tano na wajukuu wawili. Oliver Mtukudzi alianza kujihusisha na shughuli za muziki tokea 1977 na alifahamika zaidi kupitia filamu ya Neria pamoja na wimbo wa Neria mwaka 1993.

Oliver Mtukudzi alijichukulia umaarufu kupitia midundo tofauti ikiwemo Todii, wasakara, Tozeza baba, Sarawoga na nyingine nyingi.

Lulu kaibuka na mapya “Nimeamua kuuza nguo zangu nipate pesa”

Soma na hizi

Tupia Comments