Habari za Mastaa

Bill Cosby azungumza kwa mara ya kwanza sababu ya kufungwa miaka 3 jela

on

Mchekeshaji Mkongwe wa Marekani Bill Cosby (81) ambae anatumikia kifungo cha miaka mitatu mpaka 10 gerezani kwa kosa la kumnyanyasa kingono Mwanamke Andrea Constand mwaka 2004, amezungumza kwa mara ya kwanza akiwa jela.

Mchekeshaji huyo amedai kwamba imani yake ya kisiasa, vitendo vyake vya kujaribu kuweka Ubinadamu kwa Watu wa kila rangi, jinsia na dini vimemfanya afungwe jela.‬ ‪Bill amedai pia yeye ni mhanga wa ‘Mtego’ uliotengenezwa na Wanasheria wa Halmashauri wenye ‘maisha duni’ na Majaji wala rushwa lakini hata hivyo, hatokuja kujutia.‬

‪Bill alihukumiwa kwenda jela April 2018 baada ya zaidi ya Wanawake 60 kujitokeza wakidai kunyanyaswa kingono na Mchekeshaji huyo wa zamani na hukumu yake dhidi ya Constand ilichukuliwa kama ushindi kwa Wanawake hao.‬

‪Aidha Bill ambae anaamini kuwa alifungwa sio kwa sababu za kutafuta haki bali ni kwa sababu za kisiasa amesema kuwa kilichotokea kati yake na Costand ilikuwa ni makubaliano baina yao kwani Constand aliridhia.

VIDEO:DADA WA MAREHEMU GODZILLA KAFUNGUKA ‘KAACHA MTOTO MMOJA’

Soma na hizi

Tupia Comments