Michezo

Arsenal wanawasubiri Sporting CP Nov8 2018 kulinda rekodi yao

on

Katika mechi ya nne ya hatua ya makundi kwenye UEFA EUROPA League Alhamisi hii ya November 8, Arsenal itakuwa nyumbani katika uwanja wa Emirates kucheza dhidi ya Sporting CP ya Ureno, mchezo wao wa mzunguko wa kwanza Arsenal waliibuka na ushindi wa goli 1-0 ambao uliwawezesha kuongoza Kundi E.

Kwa mujibu wa mtandao wa 11v11.com unaeleza kuwa Arsenal na Sporting CP wamewahi kukutana mara tatu toka October 29 1969, Arsenal akishinda mara mbili na wametoksa sare mara moja, Fairs Cup mara mbili na mchezo wa Europa League mara moja na kesho watakutana kwa mara ya nne.

Arsenal wamekuwa katika kiwango bora na wanacheza kandanda safi tangu wampate kocha wao mpya Unai Emery ambaye amebadilisha aina ya uchezeji wake. Mchezo huo utachezwa Alhamisi ya November 8, saa 23:00  Usiku saa za Afrika Mashariki na utarushwa moja kwa moja kupitia ST World Football katika king’amuzi cha StarTimes.

Katika Usiku huo wa EUROPA mechi nyingine zitakazochezwa ni na kuoneshwa na Star Times ni pamoja na ule wa Chelsea ambao watakuwa ugenini dhidi ya BATE Borisov (saa 2:55 Usiku), Fenerbahce vs Anderlecht (saa 12:50 jioni), Lazio vs Olympique Marseille (saa 2:55 Usiku), Celtic vs RB Leipzig (saa 5:00 Usiku) na Real Betis vs AC Milan (saa 5:00 Usiku), yote kupitia chaneli za michezo za StarTimes.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments