Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

VIDEO: Erasto Nyoni kagusia kikao chao cha Manahodha (Bocco, Kaseja na Yeye) leo

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ya wachezaji wa ndani wanaowania kufuzu CHAN 2020 dhidi ya Kenya leo wamefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo, inafahamika kuwa John Bocco ndio nahodha mkuu wa kikosi cha CHAN huku Juma Kaseja akiwa nahodha msaidizi namba moja na Erasto Nyoni nahodha msaidizi namba mbili.

Kilichovutia na kushitua wengi leo ni baada ya mazoezi ya  Taifa Stars kumalizika ilionekana John Bocco, Juma Kaseja na Erasto Nyoni wakibaki watatu uwanjani kwa zaidi ya dakika zisizopungua tano na kuzungumza wao kama wao kitu ambacho waandishi walihoji kwa Erasto Nyoni ni nini kilikuwa kinajadiliwa katika mazungumzo yao yanayodaiwa kuwa ni kikao cha manahodha.

“Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu tumemaliza mazoezi ya leo salama na kuweza kujiandaa kwa mazoezi ya kesho salama, sisi wenyewe tumekaa tumejipanga vizuri na kuweza kufanya vizuri, Kenya ni timu mmoja nzuri na sisi pia ni wazuri sana tunamuomba Mungu kesho tuamke vizuri tupambane na tuweze kupata matokeo mazuri”>>>Erasto Nyoni

VIDEO: Mazoezi ya Mwisho ya Taifa Stars kabla ya kuivaa Kenya

Soma na hizi

Tupia Comments