Habari za Mastaa

Rasmi sasa R Kelly anafanyiwa uchunguzi wa kosa la Jinai

on

Muimbaji R Kelly amefikia hatua ya kufanyiwa uchunguzi wa Kosa la Jinai na Mamlaka ya mjini Georgia hii ni kutokana na filamu ya “Surviving R Kelly” iliyotayarishwa na Kampuni ya Life Time, ikiwa filamu hiyo inaonyesha baadhi ya wanawake wakiotoa ushuhuda kuhusu unyanyasaji wa kingono waliofanyiwa na nguli huyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Mwanasheria wa kitongoji cha Fulton amefungua rasmi uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa kuhusu R Kelly kupitia filamu hiyo ya Surviving R Kelly iliyoachiwa hivi karibuni na wengi kutoa mtazamo wao juu ya tukio hilo.

Inaelezwa kuwa baadhi ya mashuhuda wameshafanyiwa mahojiano na Mamlaka hiyo akiwemo mmoja ya mwanamke aliyebahatika kukimbia katika nyumba ya R Kelly ambaye anafahamika kwa jina Asante McGee.

Asante McGee

PART 4 MISUKOSUKO: ” POLISI WALIKATAA KUWA SISI SI WA SOMALI, ALILIA KAMA MTOTO”

Soma na hizi

Tupia Comments