Michezo

Surprise aliyofanyiwa Eto’o na wenzake mazoezini katika Birthday yake

on

Ukitaja soka la Afrika hakika huwezi kuacha kulitaja jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon anayeichezea Antalyspor ya Uturuki kwa sasa Samuel Eto’o kutokana na umahiri wake mkubwa uwanjani na kuitangaza vyema Afrika nje ya mipaka ya bara hili.

Samuel Eto’o leo anakumbuka kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, leo Eto’o anatimiza miaka 36 toka azaliwe March 10 1981 Doula Cameroon, Eto’o ambaye anacheza soka Antalyaspor alifanyiwa surprise na wachezaji wenzake na kumletea keki wakiwa mazoezini.

Eto’o ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa michuano ya mataifa ya Afrika AFCON akiwa na goli 18 , akiwa na Antalyaspor katika msimu wake wa kwanza alifunga goli 20 katika mechi 31 alizocheza na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya sita na kwa sasa amefunga goli 9 msimu huu katika mechi 19 alizocheza.

JIKUMBUSHE MAGOLI 20 BORA ALIYOWAHI KUFUNGA SAMUEL ETO’O

VIDEO: ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1 

Soma na hizi

Tupia Comments