Top Stories

Askari aliyeitwa kumkamata mwizi wa nguo, kaamua kumnunulia badala ya kumkamata

on


Moja ya matukio ambayo yanatokea na huenda usiamini kama kweli hutokea katika dunia hii ni pamoja na tukio hili ambalo limetokea Toronto, Canada ambako Askari aliamua kumnunulia mwizi nguo ambazo alikuwa anaiba.

Tukio hilo limetokea katika duka moja Toronto ambapo kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 kunusurika kuingia kwenye mikono ya Dola baada ya kukamatwa akiiba nguo dukani humo lakini Askari aliyeitwa kumkamata kuamua kumsamehe na kumnunulia nguo hizo.

Kwa mujibu wa Askari huyo, Niran Jeyanesan, alipigiwa simu na mfanyakazi wa duka hilo lijulikanalo kama Walmart na kupewa taarifa kuwa kijana aliiba shati, tai na soksi na alipofika eneo la tukio kijana alimueleza aliiba nguo hizo ili azivae wakati wa kwenda usaili ndipo Askari huyo aliamua kumnunulia.

>>>”Kijana huyu amekuwa akikumbwa na wakati mgumu maishani na anajaribu kutatua hilo kwa kuitafutia familia yake riziki kwa kujaribu kupata kazi.” – Jeyanesan akiiambia BBC.

Ulipitwa? Kama unatumia maji ya DAWASCO, kuna hii ya kufahamu

Soma na hizi

Tupia Comments