Michezo

Kauli ya Waziri Mwakyembe baada ya kuoneshwa ramani ya ujenzi wa uwanja wa KMC

on

Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe Jumatano ya October 2 2019 alitembelea makao makuu ya club ya KMC yaliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara hiyo waziri Mwakyembe alioneshwa ramani ya ujenzi wa uwanja wa KMC.

Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta ambaye ndio alikuwa mwenyeji wa waziri Mwakyembe alimuonesha ramani ya ujenzi wa uwanja wao mpya utakaojengwa maeneo ya Mwenge na utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 3000.

Baada ya kuona hayo na kusikia mpango wa muda mrefu wa club hiyo ni kujenga academy, waziri Mwakyembe alitoa baraka zake na kuwapongeza kwa hatua hiyo waliyofikia “Kwa uongozi wa malengo na uongozi wa pamoja ambao umefanikisha vitu vingi sana vya mfano kwa wengine”

VIDEO: Salim Kikeke kafunguka makubaliano yake na MO Dewji ubalozi wa Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments