Watafiti wameonya kuwa hali ya upofu itaongezeka kwa kasi Duniani hadi kufikia kesi Milioni 115 kufikia mwaka 2050 kama huduma za matibabu hazitaboreshwa hasa katika kuongeza Bajeti za huduma hizo.
Katika matokeo yaliyochapishwa kwenye Jarida la Lancet Global Health, Watafiti hao wamebainisha kuwa kwa sasa zipo kesi za upofu Milioni 36 Duniani kote huku vijana wakiwa kwenye hatari kubwa ya janga hili.
Idadi kubwa ya watu wenye matatizo haya imeelezwa kuwa Kusini mwa Bara la Asia na nchi za chini ya Jangwa la Sahara huku ikielezwa kuwa katika nchi 188 Duniani watu Milioni 200 wana matatizo ya kuona kuanzia katua ya kati hadi hafifu kabisa na takwimu hizi zinaonesha kupanda hadi zaidi ya Milion 550 ifikapo 2050.
Mwandishi Mkuu wa ripoti hiyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Anglia Ruskin University, Prof. Rupert Bourne amesema:>>>”Matatizo ya kuona katika hatua yoyote huwa na madhara makubwa kwa maisha ya mtu hususani katika kupunguza uwezo wao wa kujitegemea katika kufanya shughuli mbalimbali.”
Utafiti huu umetoa wito wa uwekezaji wa kutosha katika matibabu kama vile upasuaji na kuhakikisha upatikanaji wa miwani inayosaidia wenye uoni hafifu huku pia ikishauriwa kwa Serikali za nchi zinazoendelea kuboresha mifumo ya afya ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo wataalamu wa upasuaji na wauguzi ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
ULIPITWA? Play kwenye VIDEO hii chini kushuhudia MAAJABU…Tumbo limetobolewa lakini anatembea!!!